Nehemiah 7

1 aBaada ya ukuta kukamilika kujengwa upya na nikaweka milango, mabawabu wa lango, waimbaji, na Walawi waliteuliwa. 2 b , cNikamweka Hanani ndugu yangu kuwa kiongozi wa Yerusalemu, pamoja na Hanania jemadari wa ngome, kwa kuwa alikuwa mtu mwadilifu na mwenye kumcha Mungu kuliko watu wengine. 3Nikawaambia, “Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe mpaka jua litakapokuwa limepanda. Walinzi wa malango wakiwa bado kwenye zamu, waamuru wafunge milango na waweke makomeo. Pia wateueni wenyeji wa Yerusalemu wawe walinzi, kila mmoja kwenye lindo lake, na wengine karibu na nyumba zao wenyewe.”

Orodha Ya Waliorudi Toka Uhamishoni

(Ezra 2:1-70)

4 dMji ulikuwa mkubwa, tena wenye nafasi nyingi, lakini walikuwepo watu wachache ndani yake, nazo nyumba zilikuwa bado ni magofu. 5 eHivyo Mungu wangu akaweka moyoni mwangu kuwakusanya wakuu, maafisa na watu wa kawaida kwa ajili ya kuorodheshwa kulingana na jamaa zao. Nilikuta orodha ya vizazi ya wale waliokuwa wa kwanza kurudi toka utumwani. Haya ndiyo niliyokuta yameandikwa humo:

6 fHawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake,
7
In order to format the table contained in this verse correctly, it has been necessary to move the content of some adjacent verses into it.
,
hwakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Azaria, Raamia, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispereti, Bigwai, Nehumu na Baana):

Orodha ya wanaume wa Israeli ilikuwa:
 8 iwazao wa Paroshi 2,172
 9wazao wa Shefatia 372
 10wazao wa Ara 652
 11wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,818
 12wazao wa Elamu 1,254
 13wazao wa Zatu 845
 14wazao wa Zakai 760
 15wazao wa Binui 648
 16wazao wa Bebai 628
 17wazao wa Azgadi 2,322
 18wazao wa Adonikamu 667
 19wazao wa Bigwai 2,067
 20 jwazao wa Adini 655
 21wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98
 22wazao wa Hashumu 328
 23wazao wa Besai 324
 24wazao wa Harifu 112
 25wazao wa Gibeoni 95

25
In order to format the table contained in this verse correctly, it has been necessary to move the content of some adjacent verses into it.

 26 lwatu wa Bethlehemu na Netofa 188
 27 mwatu wa Anathothi 128
 28watu wa Beth-Azmawethi 42
 29 nwatu wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743
 30watu wa Rama na Geba 621
 31 owatu wa Mikmashi 122
 32 pwatu wa Betheli na Ai 123
 33watu wa Nebo 52
 34wazao wa Elamu 1,254
 35wazao wa Harimu 320
 36 qwazao wa Yeriko 345
 37 rwazao wa Lodi, Hadidi na Ono 721
 38wazao wa Senaa 3,930


39
In order to format the table contained in this verse correctly, it has been necessary to move the content of some adjacent verses into it.
tMakuhani:
wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973
 40 uwazao wa Imeri 1,052
 41 vwazao wa Pashuri 1,247
 42 wwazao wa Harimu 1,017


43Walawi:


wazao wa Yeshua (kupitia Kadmieli kupitia jamaa ya Hodavia)     74


44 xWaimbaji:


wazao wa Asafu     148


45 yMabawabu wa malango:


wazao wa

Shalumu, Ateri, Talmoni,

Akubu, Hatita na Shobai    
138


46 zWatumishi wa Hekalu:
Yaani Wanethini (pia 7:60, 73).

wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi,
47wazao wa Kerosi, Sia, Padoni,
48wazao wa Lebana, Hagaba, Shalmai,
49wazao wa Hanani, Gideli, Gahari,
50wazao wa Reaya, Resini, Nekoda,
51wazao wa Gazamu, Uza, Pasea,
52wazao wa Besai, Meunimu, Nefusimu,
53wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri,
54wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha,
55wazao wa Barkosi, Sisera, Tema,
56wazao wa Nesia na Hatifa.

57 abWazao wa watumishi wa Solomoni:
wazao wa Sotai, Soferethi, Perida,
58wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli,
59
In order to format the table contained in this verse correctly, it has been necessary to move the content of some adjacent verses into it.
wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Amoni.
 60 adWatumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392


61
In order to format the table contained in this verse correctly, it has been necessary to move the content of some adjacent verses into it.
afWafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli:
 62wazao wa

Delaya, Tobia na Nekoda
642


63 agNa kutoka miongoni mwa makuhani:
wazao wa Hobaya, Hakosi na Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo).
64Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani, kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 65 ahKwa hiyo, mtawala
Au Tirshatha: jina la heshima aliloitwa mtawala wa Yuda chini ya Ufalme wa Uajemi (pia 7:70).
aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu.
Urimu na Thumimu maana yake ni Nuru na Kweli; vifaa hivi viliwekwa kwenye kifuko cha juu cha kisibau cha kuhani mkuu ili kujua mapenzi ya Mungu kwenye mambo ya kutatanisha.


66Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 67tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 245. 68Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245 69ngamia 435 na punda 6,720.

70 akBaadhi ya viongozi wa jamaa walichangia kazi ya ujenzi. Mtawala alikabidhi kwenye hazina darkoni 1,000
Darkoni 1,000 za dhahabu ni sawa na uzito wa kilo 8.6.
za dhahabu, mabakuli 50, na mavazi 530 kwa ajili ya makuhani.
71 amBaadhi ya viongozi wa jamaa walikabidhi kwenye hazina darkoni 20,000 za dhahabu,
Darkoni 20,000 za dhahabu ni sawa na kilo 172.
na mane 2,200
Mane 2,200 za fedha ni sawa na kilo 1,300.
za fedha kwa ajili ya kazi hiyo.

72 apJumla ya matoleo ya watu wengine yalikuwa ni darkoni 20,000 za dhahabu, mane 2,000 za fedha, na mavazi sitini na saba ya makuhani.

73 aqMakuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji na watumishi wa Hekalu, pamoja na baadhi ya watu wengine na Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao wenyewe.

Ezra Asoma Sheria

Ilipotimia miezi saba, nao Waisraeli wakiwa tayari wanaishi katika miji yao,

Copyright information for SwhNEN